Thursday, January 21, 2010

Geert apandishwa kizimbani kwa kuyavunjia heshima matukufu ya Waislamu


Mbunge mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia wa Uholanzi Geert Wilders alipandishwa kizimbani jana katika mji wa Amsterdam kwa makosa kadhaa ya kuchochea machafuko ya kikaumu na kuwavunjia heshima Waislamu.Mbunge huyo pia anakabiliwa na kesi ya filamu ya Fitna ambayo imetajwa na mwendesha mashtaka wa Uholanzi kuwa ni kielelezo cha kuchochea chuki na uhasama dhidi ya Waislamu. Katika filamu hiyo ya matusi na kejeli, Wilders aliwatahadharisha Wamagharibi na kile anachodai ni kuenea kwa kasi Uislamu barani Ulaya na eti juhudi za kuifanya nchi ya Uholanzi kuwa ya Kiislamu. Vyombo vya habari vinasema kuwa mbunge huyo mwenye misimamo ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu huenda akahukumiwa kifungo cha miezi 16 jela kwa uchache na faini ya Euro elfu kumi iwapo atapatikana na hatia. Waislamu wanaunda asilimia 6 ya jamii ya watu milioni 16 ya Uholanzi.

No comments:

Post a Comment