Thursday, January 28, 2010

Hizbullah yamesema iko tayari kujibu mashambulizi ya maghasibu wa Israel

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa iko tayari kujibu mashambulizi ya aina yoyote ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Mwanachama wa Baraza la Siasa la Hizbullah Ghalib Abu Zainab amesema harakati hiyo itajibu uchokozi wa aina yoyote wa Israel katika ardhi ya Lebanon. Taarifa hiyo ya Hizbullah imetolewa baada ya Waziri wa Vita wa Israel Ehud Barak kutishia kwamba Tel Aviv itaangamiza kabisa serikali ya Lebanon iwapo kutatokea vita kati ya utawala huo ghasibu na harakati ya Hizbullah.
Ghalib Abu Zainab amejibu vitisho hivyo akisema kuwa utawala haramu wa Israel umekuwa ukitoa vitisho vya mara kwa mara kwa shabaha ya kuzusha hofu nchini Lebanon na kuvuruga usalama na amani nchini humo baada ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
Amesisitiza kuwa iwapo Israel itaanzisha mashambulizi dhidi ya Lebanon, itapata kipigo kikali.
Wakati huo huo mkuu wa jeshi la Israel Gabi Ashkenazi amelazimika kuahirisha safari yake huko Brussels Ubelgiji akihofia kutiwa nguvuni kwa kutenda jinai za vita dhidi ya binadamu wakati wa mashambulizi ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza yapata mwaka mmoja uliopita.

Kiswahili Radio - Ahmadinejad: Wamagharibi wanamuona mwanamke kama chombo cha kukidhi matakwa yao

UTAWALA WA KIFIQHI SEHEMU YA KWANZA

UTAWALA WA KIFIQHI SEHEMU YA KWANZA

UTAWALA WA KIFIQHI SEHEMU YA KWANZA

UTAWALA WA KIFIQHI SEHEMU YA KWANZA

UTAWALA WA KIFIQHI SEHEMU YA KWANZA

UTAWALA WA KIFIQHI SEHEMU YA KWANZA