Wednesday, July 2, 2014

“Umuhimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,falsafa yake pamoja na kujikurubisha zaidi ndani ya mwezi huu kwa Allah (s.w).



Sifa zote njema ni za Mwenyeezi Mungu,Mola Mlezi wa viumbe vyote.Na sala na salam ziwe kwa mwenye kubashiri na kuonya ambaye ni taa yenye kuangaza,Bwana wetu na Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w) na Ahli zake Muhammad,ambao ni bora,ni watwaharifu na ni Maasumin (a.s).Laana zote ziwe juu ya wale wote ambao ni maadui wao,kuanzia sasa mpaka itakaposimama siku ya kiyama.
Maudhui yetu itakuwa ni:Umuhimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kujikurubisha zaidi ndani ya mwezi huu kwa Allah (s.w):
Mwenyeezi Mungu (s.w) amesema:
(شَهْرُ رَمَضانَ الَّذي أُنْزِلَ فيهِ الْقُرْآنُ هُدىً لِلنَّاسِ وَ بَيِّناتٍ مِنَ الْهُدى‏ وَ الْفُرْقان)“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake Qur'an kuwa mwongozo kwa watu,na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.”
Suratul-Baqarah:Aya ya 185.
Amesema kweli Mwenyeezi Mungu,Aliye juu na Mwenye Nguvu.Ndugu yangu msomaji unayeisoma makala hii kwa muda huu,kwa hakika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni madrasa au ni shule yenye falsafa na ujumbe kwa waislaam.
Hivyo Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan tuliomo hivi leo,ni shule ya kiroho,shule ya fikra,na ni shule ya nafsi.Pia Ramadhan hii ni muhula kamili wa kukabiliana pamoja na kurekebisha yale mapungufu ya uanadamu.Kama ambavyo ni kampeni ya usafi kwa ajili ya kuchuja ule uchafu na vumbi vinavyojichanganya katika mawazo ya mwanadamu na kuzivamia fikra zake kipindi chote cha miezi kumi na moja anayoishi mwanadamu akiwa pamoja na jamii.
 
FALSAFA YA SWAUMU YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN:
 Kwa hakika mwanadamu anayeishi katika jamii kwa muda wa mwaka mmoja,huvamia au huvamiwa ndani yake na kila aina ya mazingira,na hukabiliana au hukabiliwa na kila aina ya fikra,na hujaribu au hujaribiwa na kila aina ya jaribio,na kupambana na kila aina ya pambano.
Kutokana na hayo akili ya mwanadamu,moyo wake na hisia zake,huvamiwa na kila aina ya vumbi na uchafu wa kijamii kutokana na migogoro mbalimbali ya kijamii iliyopo kila pahala,inayomkabili kila mwanadamu katika maisha haya ya dunia.
Pia mwanadamu ni mtu aliyeumbwa akiwa na silika (Instincts) mbalimbali pamoja na ile hali ya moyo wake kupenda kitu.Huenda vitu hivi vikamteka na kumzidi nguvu kwa kipindi cha mwaka mmoja.Mfano wa silika hizo ni kama vile:
Silika za kimwili (Physical instincts),silika za kujipenda na kuitanguliza nafsi yako (Instincts of self love),na silika za tamaa na khofu (Instincts of greed and fear).
Na zaidi ya hayo hatutakiwi kusahau kuwa mwanadamu amebeba nafsi hii yenye kuamrisha maovu na ambayo humuongoza mwanadamu kuelekea katika maasi na machafu na hatimae kumuweka mbali na Mola wake Mtukufu.
Na kuna silika zingine zaidi zisizokuwa kuwa hizo ambazo kwa ujumla huenda zikamteka mwanadamu na kumdhibiti.Hivyo mwanadamu hawezi kuzishinda silika hizi,na hii ni kutokana na kwamba silika hizi ni sehemu ya uwepo wa mwanadamu huyu.
Bali tunaweza kuongezea katika hayo nukta hii ifuatayo kwamba:Kila mwanadamu anae shetani wake (Every one has a demon or devil) ambaye humtaka mwanadamu apotoke na kuwa mbali na Mola wake Mtukufu.Na hii ni nukta muhimu aliyoiashiria Bwana Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliposema:
(ما من إنسان إلا ومعه شيطان)(Hakuna mwanadamu ispokuwa analo pepo).Rejea:Biharul-Anwaar:Juzuu ya 17.Ukurasa wa 44.Mlango wa 15.Huenda mwanadamu akajidanganya na kudhani kwamba yeye ni shujaa,hawezi kuathiriwa na uchafu huu wa kijamii unaomzunguka pamoja na silika hizi mbalimbali anazizobeba,pia huenda akajiona kuwa yeye ni mtu mwenye nguvu katika maamuzi yake,mjanja na aliye imara zaidi kiimani!.
Lakini pamoja na hayo yote,kwa vyovyote vile atakavyokuwa mwenye nguvu katika maamuzi yake,kwa vyovyote vile atakavyokuwa imara na mwerevu,hatokosa kuathiriwa na hali hiyo kama anavyo athirika (according to the presence of large number of poisonous ideas,deviation and various currents in society) kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya fikra zenye sumu,upokokaji na mikondo mbalimbali katika jamii.Hayo yote huwaelekeza zaidi wanadamu walio wengi katika mambo ya kimaada na kuwaweka mbali zaidi na mambo ya kimaanawi kama vile kuwaweka mbali zaidi na Mwenyeezi Mungu (s.w).
Hivyo mwingiliano huu wa kijamii (Social Interaction),husababisha kupotoka kwa mwanadamu huyu akiwa ni mwenye kuhisi na kutaka,au la,bali akiwa ni mwenye kuchukia na kutohisi.
Hivyo,mwanadamu huyu anayeishi katika jamii yenye hali kama hii,anatakiwa kuwa na kitu kitakacho muhifadhi,au kinga imara itakayoweza kumuhifadhi ili asiweze kuwa chini ya shubha hizi na misukosuko hii pamoja na misukumo hii isiyokuwa ya kimantiki inayoambatana na silika hizo tulizozitaja ambazo hupenda kumuongoza mwanadamu kuelekea njia isiyokuwa sahihi,nayo ni njia ya upotokaji na uasi.
Hivyo Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan,ni kinga ya kipekee na ni ngome imara itakayoweza kumhifadhi na kumuokoa mwanadamu huyu asikumbwe na janga la upotokaji wala kuguswa na uchafu mbalimbali wa kijamii unaopatikana katika jamii zetu zilizojaa upotokaji na uovu wa kila aina.
Pia mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan,unazidhibiti silika za mwandamu na kuziwekea mipaka,ili asiweze kupotoka na kwenda kinyume na njia sahihi iliyowekwa na Uislaam.
So,this month is a period of meditation and reflection,also it is a month which gurantees a guidance to (human being) the straight path.And that’s the Holy Qur’an.
Kwa ibara nyingine tunaweza kusema kwamba:Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan unachukuliwa kuwa ni Mwezi wa kutafakari zaidi na kufikiria,pamoja na kuihesabu nafsi yako.Kama ambavyo ni Mwezi unaompa mwanadamu uhakika wa Mwogozo kuelekea katika njia sahihi na ya haki.Na hiyo ni Qur’an Tukufu.
Na imekuja katika Hadithi kutoka kwa Ibn Hisha’m bin Al-Hakam kwamba alimuuliza Aba Abdillah Al-swaadiq (a.s) kuhusiana na sababu ya kuwepo kwa swaumu.Imam Swadiq (a.s) akasema:
(إنما فرض الله الصيام ليستوي به الغني والفقير: وذلك أن الغني لم يكن يجد مس الجوع فيرحم الفقير لأن الغني كلما أراد شيئاً قدر عليه ‘،فأراد الله تعالى أن يسوي بين خلقه ‘وأن يذيق الغني الجوع والألم ليرق على الضعيف ويرحم الجائع.)Kwa hakika Mwezi Mungu (s.w) amefaradhisha Swaumu ili kwa swaumu hiyo Tajiri aweze kuwa sawa na Maskini:Na hilo ni kwa sababu (kusingelikuwepo na swaumu,basi kwa hakika) Tajiri asingeweza kuhisi wala kuguswa na njaa,na hivyo ingelikuwa ni vigumu kwake yeye kumhurumia masikini (kutokana na kwamba yeye kama Tajiri hajui hali ya umasikini na tabu zake vinafananaje),maana Tajiri kila kitu akitakacho,basi ana uwezo wa kukipata,(lakini masikini hawezi kupata kila kitu anachokihitajia na kukitamani,maisha yake siku zote ni maisha ya tabu,shida na njaa),hivyo Mwenyeezi Mungu (s.w) akataka kulinganisha baina ya waja wake,na kumuonjesha Tajiri njaa pamoja na maumivu,ili awe na huruma kwa aliye dhaifu na mnyonge,na amhurumie mwenye maisha ya shinda na njaa (Masikini).

RAMADHAN NI MWEZI WA KUJIKURUBISHA ZAIDI KWA ALLAH (S.W):
Kulingana na ufafanuzi uliopita,dini ya Uislaam imefaradhisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ili uweze kuwa Mwezi wa Ibada na Mwezi wa kukata mahusiano na dunia pamoja na vitu vyote vya kimaada vinavyomshughulisha mwanadamu na kumuweka mbali na Mola wake Mtukufu.
Pia ni Mwezi Mtukufu unaomtaka mwandamu ajitahidi zaidi na zaidi katika kuzichuma thawabu zinazopatikana ndani ya Mwezi yake.Ni Mwezi ambao imesisitizwa sana kuisoma Qur’an ndani yake ambapo kuisoma Aya moja tu ya Qur’an Tukufu katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan,thawabu zake ni sawa na kuzisoma Aya sabini,au ni sawa na kuisoma Qur’an mzima katika masiku ya kawaida yasiyokuwa masiku ya Mwezi wa Mwezi Mtukufu Ramadhan.
(So,when you recite one verse of the Holy Qur’an in the Holy Month of Ramadan is like reciting seventy Verses, or to recite the whole Qur’an in other months).Pia Mwezi huu unamuelekeza zaidi mwanadamu katika kuzisoma dua mbalimbali,na umemuwekea dua maalum kulingana na nyakati ambapo kila wakati una dua yake Mahsusi.
Pia Uislaam umemtaka mwanadamu katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan kuwa na tabia mzuri,kusamehe,kufanya ihsani,kuendeleza udugu na kupendana kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu (s.w).Na ukaweka thawabu za kila jema kuwa ni mara mbili yake ili ile hali ya kuchukiana inayomvamia mwanadamu na kuyatawala maamuzi yake iweze kutoweka na kupotea.
Na kwa mujibu wa maneno haya tunaweza kunyumbua nukta hii muhimu kwamba swaumu hii inayoathiri katika Roho ya mwanadamu na kumbadilisha mwanadamu kutoka hali isiyostahiki hadi kumfikisha katika hali inayostahiki na ya kusifika mbele ya Allah (s.w),swaumu ambayo tumesema kuwa ni kinga na ngome imara inayomhifadhi mwanadamu na kumuokoa na upotokaji pamoja na uasi….kwa hakika maana yake sio kujizuia kula na kunywa tu basi,bali maana ya Swaumu hii ni kama alivyoielezea Imam Jaafar Swadiq (a.s) aliposema:
(إن الصيام ليس من الطعام والشراب وحده،ثم قال)
 “Hakika ya swaumu sio tu kujizuia kula na kunywa basi,kisha akasema:
قالت مريم:(إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمنِ صَوْما):يعني صوماً و صمتاً،فإذا صمتم فاحفظوا ألسنتكم ‘وغضوا أبصاركم ‘ولا تنازعوا ولا تحاسدوا.قال:وسمع رسول الله  (ص) امرءة تسب جارية لها وهي صائمة.فدعى رسول الله (ص) بطعام فقال لها:كلي،فقالت: إني صائمة،فقال (ص):كيف تكونين صائمة وقد سببْتِ جاريتَكِ ؟! . إن الصوم ليس من الطعام والشراب فقط.م قال الإمام الصادق (ع):إذا صمتم فاليصم سَمْعُكُم وبصَرُكُمْ من الحرام والقبيح ودع المراء و أذى الخادم،وليكن عليك وقار الصائم،ولا تجعل يوم صومك كيوم فطرك
.
Amesema Maryam (s.a):
” Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga”.Rejea:Surat Maryam:Aya ya 26.Kwa maana kufunga na kunyamaza,hivyo mkifunga chungeni ndimi zenu,na fumbeni (chungeni) macho yenu,na msizozane wala kufanyiana husda.
Akaendelea kusimulia Hisham bin Hakam kwamba amesema Imam Swadiq (a.s) kuwa siku moja:Mtume (s.a.w.w) alimsikia Mwanamke akimtukana mjakazi wake huku mwanamke huyo akiwa amefunga.Mtume (s.a.w.w) akaitisha chakula,kisha akamwambia mwanamke huyo:Kula !.Mwanamke huyo akasema:Mimi nimefunga!.
Mtume (s.a.w.w) akasema:Vipi wewe unadai umefunga hali ya kuwa unamtukana mjakazi wako?!.Kwa hakika kufunga sio kujizuia kula na kunywa tu.
Kisha akasema Imam Swadiq (a.s):Ukifunga basi nayafunge masikio yako na macho yako kwa kuepukana na mambo ya haram na mabaya,na jiepushe unafiki (Avoid Hypocrisy)
na kumuudhi mtumishi (Don't harm  a server),na jitahidi iwe juu yako uchamungu wa yule mtu aliyefunga,na kamwe usiifanye siku yako ya kufunga iwe kama siku ya kula kwako.Mwisho wa makala yetu kuhusiana na “Umuhimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,falsafa yake pamoja na kujikurubisha zaidi ndani ya mwezi huu kwa Allah (s.w).
Mwandishi wa makala hii : Taqee Zachalia.

Karibu tena kwa makala zaidi,makala murwa na zilizojaa faida.

Wednesday, February 10, 2010

Mgosi: Wenger mnunue Rooney ili (kuiokoa arsenal).

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema wataongeza nguvu maradufu kuanzia mechi ya leo Jumanne dhidi ya Manyema lakini akamshauri Arsene Wenger kuwa: "Tunamuhitaji Wayne Rooney wa Manchester United."

Mgosi, ambaye ni shabiki wa Arsenal aliyekerwa na vipigo viwili ilivyopata timu hiyo dhidi ya Manchester United mabao 3-0 na mabao 2-0 kutoka kwa Chelsea juzi Jumapili alidai kuwa wataifunga Liverpool kesho Jumatano.
"Kwa upande wa Simba tumejipanga vizuri sana na kuanzia mechi na Manyema tunaingia na nguvu mpya kabisa ambayo itakuwa ni zaidi ya mechi zilizopita," alisema Mgosi ambaye timu yake imepiga kambi kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.

"Tumeamua kutumia nguvu zaidi kwavile tumegundua kwamba timu zimetupania sana kila tunapokanyaga ndio maana hata Kagera Sugar walipotoa sare na sisi wamefurahia sana, hivyo tumeamua kujidhatiti upya.

 "Hatutaki kuvuruga rekodi yetu na sidhani kama yaliyotokea Kagera yatajitokeza tena. Mashabiki wetu watupe sapoti na wasiwe na wasiwasi kwani tutafanya kazi."
Akizungumzia Arsenal, Mgosi alisema; "Arsenal tuko vizuri tunacheza mpira unaonekana kuanzia mwanzo, lakini tatizo hatuna mtu wa kutumbukiza kwenye nyavu."
"Mipira inakwenda vizuri kabisa tena kwa ufundi wa hali ya juu mpaka eneo la hatari, lakini hakuna wa kufunga, tunamhitaji mshambuliaji kama Jermain Defoe wa Tottenham au Wayne Rooney wa Manchester United, Kocha Arsene Wenger anahitaji kuliangalia hilo.
"Lakini ukiangalia pia kucheza mechi mfululizo na hizo timu kubwa nne ni tatizo, tumetoka Manchester hatujatulia tumekwenda kwa Chelsea sasa tunakwenda Liverpool hizo zote ni mechi ngumu sana na timu ikiteleza mechi moja ni rahisi sana kupoteza na inayofuata."

"Liverpool hawatuwezi, wale ni saizi yetu wanasuasua sana, hapa juzi juzi wamebahatisha tu kushinda lakini hawatufungi sisi Arsenal."
Lakini kocha wa Arsenal ni kama vile amemjibu Mgosi kwani jana Jumatatu aliiambia televisheni ya klabu hiyo kwamba; "Tulimiliki mpira vizuri sana lakini tulishindwa kuigeuza hali hiyo iwe ya ushindi wa mabao."

"Halafu wao wana uzoefu kuliko sisi, wale wana wastani wa miaka 29 sisi tuna kikosi cha wastani wa umri wa miaka 23. Ukicheza na hizi timu ukapoteza mchezo mmoja kisaikolojia ni madhara kwa mechi inayofuata, mechi ya Liverpool ni ngumu kama ilivyokuwa kwa Chelsea, lakini siwezi kukata tamaa tutapambana kama kawaida."